Sehemu ya kwanza:
Kwa jina naitwa yohana maduhu,nimkazi wa mwanza..katika
maisha yangu nimekuwa na imani kubwa na shughuli za kilimo na ufugaji kama ndio
chanzo chepesi zaidi cha kujipatia kipato halali,japo mtu anaweza kuamini
tofauti na ninavyo amini mimi…tatizo kubwa lililopo kwa wakulima wengi ni
kutokujua thamani ya kazi yao hivyo wafanyabiashara wengi wamekuwa wakinunua
bidhaa zao kwa bei ya chini sana harafu wao wanauza kwa bei ya juu.Mfano
chungwa moja la wastani linaweza kuuzwa sokoni kwa shilingi mia mbili,wakati
mlanguzi kanunua kwa mkulima machungwa kumi ya aina hiyo kwa shilingi mia
mbili,huo ni mfano mdogo tu,japo muuzaji wa sokoni analipa ushuru lakini ushuru
huo ni mdogo tu ambao hata mkulima anaweza kustahimili kuulipa.
Nilikuwa sijawahi kufanya kilimo chochote katika maisha
yangu,ila nikadhamilia kuingia katika kilimo kwa lengo la kupata faida ya juu
kabisa(maximum profit)ya kile ntakachozalisha.na wazo langu likanipeleka
kufanya kilimo cha matikiti maji.na sababu ya kuchagua matikiti maji ni kama
ifuatavyo: kwanza kabisa yanakomaa kwa muda mfupi,(miezi miwili hadi
mitatu)hivyo sitasubili saana kupata faida yangu,pili ni matunda ambayo watu
wengi wanayapenda,mimi nikiwa mmoja wao. Lakini pia nilitamani sana
nisikosee,hivyo nilidhamilia kuhusisha wataaramu katika kila hatua ikiwa ni
pamoja na kusoma kwenye mitandao habari mbalimbali zinazohusu kilimo cha
matikiti maji. Nilifuata hatua zifuatazo:
HATUA YA KWANZA.
kutafuta shamba.
Hii ilikuwa ni hatua ya kutafuta shamba ,nilikwenda sehemu
moja inaitwa usagala,nje kidogo ya jiji la mwanza na kukodi shamba la heka tatu
kwa kiasi cha shilingi laki moja (kubargain muhimu) .kwa kuzingatia ukaribu na uwepo
wa vyanzo vya maji.pia nilizingatia aina ya udongo kwa vile nilishajua matikiti
maji yanastawi vizuri zaidi katika ardhi ya kichanga na sababu kubwa ikiwa ni
kutotuamisha maji kwa ardhi ya kichanga.kwani maji yakiwa yanatuama husababisha
matunda kuoza.
Nikiwa shambani kuhakikisha kama linafaa kwa kilimo cha matikiti
Nikiwa tayari kwa ajiri ya maandalizi ya kilimo
HATUA YA PILI
Hii ilikuwa ni hatua ya kuandaa shamba,niliajiri wanakijiji
wakalima eneo lote la heka tatu kwa kutumia maksai,pamoja na majembe ya mkono
kwa ajili ya kupanga matuta.hatua hii ilinighalimu kiasi cha shilingi laki moja
na nusu.hapa maksai wanatifua aldhi harafu majembe ya mkono yanatengeneza
matuta(kama kawa nililia shida nikapunguziwa).
Ili kazi iende vizuri
nilifanya mpango tukawa tunapika chakula na kila mtu alikuwa anafurahi.hii
inasaidia kupunguza movements wakati wa kazi,na pia inawatia moyo wafanyakazi na zaidi ikanijengea uhusiano mzuri na wao.wakati mwingine tatizo
linaweza kutokea,wanakuwa upande wako.
HATUA YA TATU
upandaji
Katika
ununuzi wa mbegu kwa mara ya kwanza ndo nilikutana na neno highbreed(mbegu chotara,zilizo
tengenezwa kitaaram kutoa mazao mengi na bora)sikuweza kununua mbegu hizo kwa
vile zilikuwa na gharama kubwa na mimi kwa vile ndo kilimo cha kwanza sikutaka
kuingia gharama kubwa kwa kitu ambacho sijui matokeo yake(japo sikushauri
ufanye kama mimi).niliamua kununua mbegu ya kawaida aina ya sugar
baby,inayokomaa kwa siku sabini hadi themanini.pia matunda yake yanaukubwa wa
wastani,hapa niligharamika kiasi cha shilingi elfu hamsini kwa ajiri ya
manunuzi ya mbegu.katika upandaji tulikuwa tunaweka mbolea ya samadi iliyooza
vizuri kwenye kila shimo na kuichanganya vizuri na udongo,tulihakikisha tuna panda mbegu mbili mbili kila shimo umbali wa sentimita mbili chini ya udongo kwa umbali wa sentimita 30 toka shina hadi shina na mita 1.5-2 kutoka mstari hadi mstari, kwavile wanakijiji washakuwa rafiki zangu
walinipandia mbegu bila gharama yeyote,kuwaonesha ninajari nikaungurumisha
ugali wa maana na dagaa za kutosha tukala tukashiba,na burudani za hapa na pale
hazikukosa.
INAENDELEA....