Monday, 15 February 2016

NILIPOFANYA KILIMO CHA MATIKITI MAJI KWA MARA YA KWANZA

Sehemu ya tano(mwisho)

UVUNAJI WA MATUNDA

Baada ya siku sabini tulisitisha umwagiliaji katika shamba letu kwa muda wa wiki moja kabla ya uvunaji,hii inasaidia kufanya matunda yajitengenezee sukari na kuyafanya kuwa matamu zaidi,pia inasaidia kuepusha kupasuka kwa matunda.Huu ni ushauri ambao tulipewa na Bwana shamba.
Baada ya siku sabini na tano(unaweza kuenda mpaka siku themanini)shamba letu lilikuwa tayari kwa ajiri ya kuvuna na tulianza shughuli ya uvunaji.
Kilichonishangaza na kunifurahisha ni kwamba siku ya uvunaji nilipata kampani kubwa sana kuliko kipindi chote,karibu kijiji kizima kilikuja kunisaida kuvuna,watoto kwa wazee.

                                          vijana wakivuna matikiti maji shambani



picha za juu,vijana wakipakia matikiti maji kwenye gari tayari kwa kupeleka sokoni


SOKO
Wakati wa kuvuna mazao yetu walikuja wafanyabiashara mbalimbali kutaka kununua mazao yote.Hawa jamaa kwa kawaida humpunja mkulima ili wao wapate faida kubwa zaidi(mpaka mara tatu au nne ya bei waliyonunulia).Hivyo sisi tulikuwa tumejipanga kuuza wenyewe sokoni.Tulikodisha canter mbili tukasomba mzigo wote na kuupeleka katika soko la Buhongwa ambalo ni karibu zaidi.Tuliomba nafasi kwenye uongozi wa soko na kuweka bidhaa zetu na kuanza kuuza kwa jumla na rejareja na mimi mwenyewe nikiwa msimamizi mkuu.Kwavile kulikuwa na uhaba wa matikiti maji sokoni kwa kipindi hicho tuliweza kumaliza mzigo wetu ndani ya wiki moja tu na mauzo yetu yalikuwa ni jumla ya shilingi millioni nane.Gharama zote nilizotumia hazikufika millioni moja.Hivyo basi nilitengeneza shillingi millioni saba kwa muda wa miezi mitatu tena kwa kilimo nilichokifanya kwa mara ya kwanza na pasipo uzoefu wowote.
KAMA UNATAKA MALI UTAYAPATA SHAMBANI.

3 comments:

  1. Aksante ndg. Maduhu kwa simulizi nzuri na ya kufundisha, Mimi nimepata kitu na nitakifanyia kazi

    ReplyDelete
  2. Aksante ndg. Maduhu kwa simulizi nzuri na ya kufundisha, Mimi nimepata kitu na nitakifanyia kazi

    ReplyDelete
  3. Asante Sana ndugu maduhu hakika umetufumbua macho vijana wenzio .kwasasa najipanga nakufanya jamno hilo ifikapo February 2017...nafikiri ntaitaji kujua mengi saaana juu ya ukulima wa tikiti kutoka kwako pia soko zima kwaujumla email yangu hii hapa naomba tuwasiliane plz radhiarambat@gmail.com.

    ReplyDelete