Saturday 6 June 2015

NILIAPOFANYA KILIMO CHA MATIKITI MAJI KWA MARA YA KWANZA. Na yohana maduhu

Sehemu ya kwanza:
Kwa jina naitwa yohana maduhu,nimkazi wa mwanza..katika maisha yangu nimekuwa na imani kubwa na shughuli za kilimo na ufugaji kama ndio chanzo chepesi zaidi cha kujipatia kipato halali,japo mtu anaweza kuamini tofauti na ninavyo amini mimi…tatizo kubwa lililopo kwa wakulima wengi ni kutokujua thamani ya kazi yao hivyo wafanyabiashara wengi wamekuwa wakinunua bidhaa zao kwa bei ya chini sana harafu wao wanauza kwa bei ya juu.Mfano chungwa moja la wastani linaweza kuuzwa sokoni kwa shilingi mia mbili,wakati mlanguzi kanunua kwa mkulima machungwa kumi ya aina hiyo kwa shilingi mia mbili,huo ni mfano mdogo tu,japo muuzaji wa sokoni analipa ushuru lakini ushuru huo ni mdogo tu ambao hata mkulima anaweza kustahimili kuulipa.
Nilikuwa sijawahi kufanya kilimo chochote katika maisha yangu,ila nikadhamilia kuingia katika kilimo kwa lengo la kupata faida ya juu kabisa(maximum profit)ya kile ntakachozalisha.na wazo langu likanipeleka kufanya kilimo cha matikiti maji.na sababu ya kuchagua matikiti maji ni kama ifuatavyo: kwanza kabisa yanakomaa kwa muda mfupi,(miezi miwili hadi mitatu)hivyo sitasubili saana kupata faida yangu,pili ni matunda ambayo watu wengi wanayapenda,mimi nikiwa mmoja wao. Lakini pia nilitamani sana nisikosee,hivyo nilidhamilia kuhusisha wataaramu katika kila hatua ikiwa ni pamoja na kusoma kwenye mitandao habari mbalimbali zinazohusu kilimo cha matikiti maji. Nilifuata hatua zifuatazo:
HATUA YA KWANZA.
kutafuta shamba.
Hii ilikuwa ni hatua ya kutafuta shamba ,nilikwenda sehemu moja inaitwa usagala,nje kidogo ya jiji la mwanza na kukodi shamba la heka tatu kwa kiasi cha shilingi laki moja (kubargain muhimu) .kwa kuzingatia ukaribu na uwepo wa vyanzo vya maji.pia nilizingatia aina ya udongo kwa vile nilishajua matikiti maji yanastawi vizuri zaidi katika ardhi ya kichanga na sababu kubwa ikiwa ni kutotuamisha maji kwa ardhi ya kichanga.kwani maji yakiwa yanatuama husababisha matunda kuoza.

            Nikiwa shambani kuhakikisha kama linafaa kwa kilimo cha matikiti

Nikiwa tayari kwa ajiri ya maandalizi ya kilimo

HATUA YA PILI
Hii ilikuwa ni hatua ya kuandaa shamba,niliajiri wanakijiji wakalima eneo lote la heka tatu kwa kutumia maksai,pamoja na majembe ya mkono kwa ajili ya kupanga matuta.hatua hii ilinighalimu kiasi cha shilingi laki moja na nusu.hapa maksai wanatifua aldhi harafu majembe ya mkono yanatengeneza matuta(kama kawa nililia shida nikapunguziwa).

Ili  kazi iende vizuri nilifanya mpango tukawa tunapika chakula na kila mtu alikuwa anafurahi.hii inasaidia kupunguza movements wakati wa kazi,na pia inawatia moyo wafanyakazi na zaidi ikanijengea uhusiano mzuri na wao.wakati mwingine tatizo linaweza kutokea,wanakuwa upande wako.

HATUA YA TATU
upandaji
Katika ununuzi wa mbegu kwa mara ya kwanza ndo nilikutana na neno highbreed(mbegu chotara,zilizo tengenezwa kitaaram kutoa mazao mengi na bora)sikuweza kununua mbegu hizo kwa vile zilikuwa na gharama kubwa na mimi kwa vile ndo kilimo cha kwanza sikutaka kuingia gharama kubwa kwa kitu ambacho sijui matokeo yake(japo sikushauri ufanye kama mimi).niliamua kununua mbegu ya kawaida aina ya sugar baby,inayokomaa kwa siku sabini hadi themanini.pia matunda yake yanaukubwa wa wastani,hapa niligharamika kiasi cha shilingi elfu hamsini kwa ajiri ya manunuzi ya mbegu.katika upandaji tulikuwa tunaweka mbolea ya samadi iliyooza vizuri kwenye kila shimo na kuichanganya vizuri na udongo,tulihakikisha tuna panda mbegu mbili mbili kila shimo umbali wa sentimita mbili chini ya udongo kwa umbali wa sentimita 30 toka shina hadi shina na mita 1.5-2 kutoka mstari hadi mstari, kwavile wanakijiji washakuwa rafiki zangu walinipandia mbegu bila gharama yeyote,kuwaonesha ninajari nikaungurumisha ugali wa maana na dagaa za kutosha tukala tukashiba,na burudani za hapa na pale hazikukosa.




INAENDELEA....

Tuesday 2 June 2015

KUTANA NA MFUGAJI ALIYEANZA KWA KUSOMA KITABU CHA UJASILIAMALI HADI KUWA MFUGAJI MKUBWA

"Baada ya kuona maisha yanakuwa magumu,niliumiza kichwa  nifanye shughuli gani ili niongeze kipato changu,hivyo nikaamua kununua kitabu cha ujasiliamali na kujifunza kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji"....haya ni maneno ya bwana Alfonce Emmanuel ambae ni mkazi wa jijini Mwanza maeneo ya kiseke.

Bwana alfonce akilisha kuku zake

 Akiendelea kutufahamisha jinsi alivyoanza shughuli za ufugaji Bwana alfonce anasema alianza na kuku wanane tu,saba wakiwa majike na jogoo mmoja ambao aliwanunua kwa umakini wa kuzingatia mbegu bora kutoka kwa jirani yake ambae nae alikuwa mfugaji
lakini nini cha tofauti kwa alphonce ni jinsi ya yeye anavyo wapata kuku wake." mimi na totolesha kuku mwenyewe kwa kuwapa matetea mayai na wiki moja baada ya vifaranga kutotolewa navitoa kwa matetea na kuwa weka katika chumba ambacho watapata joto lakutosha na kukua wakati huo nawapa pumba laini ama chenga ndogondogo sana za mchele na katika maji yao nawachanganyia vitamini na groucouse  "alisema  alphonce.

Chumba cha kuhifadhia vifaranga wa wiki moja hadi mwezi mmoja

"baada ya mwezi mmoja navichukua vifaranga na kuviweka katika mabanda katika chumba kingine, chumba hiki kimegawanyika katika mabanda mawili ikiwa ni moja kwajili ya kuku wa mwezi mmoja na lingine mwenzi wa pili wakati kuku walioko chini ya mabanda haya ni kuku walio zidi miezi mitatu amabao wako tayari kuchanganywa na kuku wengine wakubwa. nafanya hivi kwa sababu ya kuwaepusha kuku na magonjwa, maana kama vifaranga vya mwenzi mmoja havina kinga ya mwili ya kutosha hivyo ukiviweka na kuku wakubwa ni rahisi kupata magonjwa na kufa". alphoince.

Chumba cha vifaranga wa mwezi mmoja hadi miwili.

"huwa natumia chakula cha kawaida kwa maana ya pumba za mahindi, mchicha na dagaa pamoja na vyakula vingine vya kuku kama konokono na mashudu.
lakini changamoto kubwa ni magonjwa ya kuku,kila baada ya miezi mitatu huwa nawapa chanjo ya kideli ambayo ni Newcastle. pia kwa vifaranga huwa nawapa chanjo ya ndui mara tu wafikishapo wiki mbili.pamoja na hayo najitahidi kuwatibu pale wanapopata magonjwa kama mafua kwa kuwapa dawa za mafua kama vile fluban.kwa kifupi nakuwa karibu zana na mifugo yangu hiyo ili kujua tatizo..vilevile ninapogundua kunakuku anaugonjwa huwa namtenganisha na wengine ili asiwaambukize.
kutokana na uzoefu nilionao kwa sasa ninauwezo wa kupambanua magonjwa ya kuku kwa kuangalia aina ya kinyesi cha kuku na hata muonekano wa kuku.mfano kinyesi kikiwa cha kijani basi kuku anatatizo la mafua,japo kwa tatizo hilohilo kuku anaweza kua anapiga chafya.na ni bora mfugaji yeyote kuyajua magonjwa ya kuku na dawa zake.".



kwa kiasi kikuibwa faida yake inatokana na kuuza kuku na mara nyingine kuuza mayai japo bwana alfonce yeye anadai hauzi mayai,ila anachofanya ni kuyatotoresha ili awe na kuku wengi. kuku moja mkubwa anauza 10000 kwa mtetea na 15000 kwa jogoo japo bei huongezeka kipindi cha sikukuu.zaidi huwauza  kuku hao kwa jumla kwa wafugaji wengine. 

Sunday 24 May 2015

KARIBUNI KATIKA BLOG hii

Karibuni wadau mbalimbali wa  kilimo na  ufugaji,na hata wanaopenda kujifunza kuhusu mambo haya. nina imani watajifunza mambo mengi yanayohusiana na kilimo na ufugaji,na kikubwa zaidi ni jinsi ya kupata faida kutokana na kilimo na ufugaji..Karibuni sana.

..