Tuesday 2 June 2015

KUTANA NA MFUGAJI ALIYEANZA KWA KUSOMA KITABU CHA UJASILIAMALI HADI KUWA MFUGAJI MKUBWA

"Baada ya kuona maisha yanakuwa magumu,niliumiza kichwa  nifanye shughuli gani ili niongeze kipato changu,hivyo nikaamua kununua kitabu cha ujasiliamali na kujifunza kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji"....haya ni maneno ya bwana Alfonce Emmanuel ambae ni mkazi wa jijini Mwanza maeneo ya kiseke.

Bwana alfonce akilisha kuku zake

 Akiendelea kutufahamisha jinsi alivyoanza shughuli za ufugaji Bwana alfonce anasema alianza na kuku wanane tu,saba wakiwa majike na jogoo mmoja ambao aliwanunua kwa umakini wa kuzingatia mbegu bora kutoka kwa jirani yake ambae nae alikuwa mfugaji
lakini nini cha tofauti kwa alphonce ni jinsi ya yeye anavyo wapata kuku wake." mimi na totolesha kuku mwenyewe kwa kuwapa matetea mayai na wiki moja baada ya vifaranga kutotolewa navitoa kwa matetea na kuwa weka katika chumba ambacho watapata joto lakutosha na kukua wakati huo nawapa pumba laini ama chenga ndogondogo sana za mchele na katika maji yao nawachanganyia vitamini na groucouse  "alisema  alphonce.

Chumba cha kuhifadhia vifaranga wa wiki moja hadi mwezi mmoja

"baada ya mwezi mmoja navichukua vifaranga na kuviweka katika mabanda katika chumba kingine, chumba hiki kimegawanyika katika mabanda mawili ikiwa ni moja kwajili ya kuku wa mwezi mmoja na lingine mwenzi wa pili wakati kuku walioko chini ya mabanda haya ni kuku walio zidi miezi mitatu amabao wako tayari kuchanganywa na kuku wengine wakubwa. nafanya hivi kwa sababu ya kuwaepusha kuku na magonjwa, maana kama vifaranga vya mwenzi mmoja havina kinga ya mwili ya kutosha hivyo ukiviweka na kuku wakubwa ni rahisi kupata magonjwa na kufa". alphoince.

Chumba cha vifaranga wa mwezi mmoja hadi miwili.

"huwa natumia chakula cha kawaida kwa maana ya pumba za mahindi, mchicha na dagaa pamoja na vyakula vingine vya kuku kama konokono na mashudu.
lakini changamoto kubwa ni magonjwa ya kuku,kila baada ya miezi mitatu huwa nawapa chanjo ya kideli ambayo ni Newcastle. pia kwa vifaranga huwa nawapa chanjo ya ndui mara tu wafikishapo wiki mbili.pamoja na hayo najitahidi kuwatibu pale wanapopata magonjwa kama mafua kwa kuwapa dawa za mafua kama vile fluban.kwa kifupi nakuwa karibu zana na mifugo yangu hiyo ili kujua tatizo..vilevile ninapogundua kunakuku anaugonjwa huwa namtenganisha na wengine ili asiwaambukize.
kutokana na uzoefu nilionao kwa sasa ninauwezo wa kupambanua magonjwa ya kuku kwa kuangalia aina ya kinyesi cha kuku na hata muonekano wa kuku.mfano kinyesi kikiwa cha kijani basi kuku anatatizo la mafua,japo kwa tatizo hilohilo kuku anaweza kua anapiga chafya.na ni bora mfugaji yeyote kuyajua magonjwa ya kuku na dawa zake.".



kwa kiasi kikuibwa faida yake inatokana na kuuza kuku na mara nyingine kuuza mayai japo bwana alfonce yeye anadai hauzi mayai,ila anachofanya ni kuyatotoresha ili awe na kuku wengi. kuku moja mkubwa anauza 10000 kwa mtetea na 15000 kwa jogoo japo bei huongezeka kipindi cha sikukuu.zaidi huwauza  kuku hao kwa jumla kwa wafugaji wengine. 

3 comments:

  1. je nikiitaji hao kuku mkoani unaweza kunitumia??

    ReplyDelete
  2. Ebana ningependa kufahamu "nilipofanya kilimo cha matikiti maji kwa mara ya kwanza sehemu ya pili" plz

    ReplyDelete
  3. Du braza!!! ume share nasi vizuri sana nimejifunza kitu tena na picha juu tunashukuru kwa moyo wako, we si mchoyo nilikuwa na wazo kama lako ila nikawa na maswali mengi ambayo hayana majibu, hii blog yako imenisaidia kujibu maswali yangu. Mimi binafsi nina ka eneo lilikuwa poli nimeanza na kuweka mkuza ( kuweka mpaka uonekane kati ya shamba moja na jingine)then nitasafisha shamba ili baadaye nipande matikiti, ingawa bado nina changamoto kichwani, ulinzi wa shamba? ngedele, nguruwe, V baka? ila kwa kuanzia si mbaya, Nashukuru. wakora muno

    ReplyDelete