Saturday 6 June 2015

NILIAPOFANYA KILIMO CHA MATIKITI MAJI KWA MARA YA KWANZA. Na yohana maduhu

Sehemu ya kwanza:
Kwa jina naitwa yohana maduhu,nimkazi wa mwanza..katika maisha yangu nimekuwa na imani kubwa na shughuli za kilimo na ufugaji kama ndio chanzo chepesi zaidi cha kujipatia kipato halali,japo mtu anaweza kuamini tofauti na ninavyo amini mimi…tatizo kubwa lililopo kwa wakulima wengi ni kutokujua thamani ya kazi yao hivyo wafanyabiashara wengi wamekuwa wakinunua bidhaa zao kwa bei ya chini sana harafu wao wanauza kwa bei ya juu.Mfano chungwa moja la wastani linaweza kuuzwa sokoni kwa shilingi mia mbili,wakati mlanguzi kanunua kwa mkulima machungwa kumi ya aina hiyo kwa shilingi mia mbili,huo ni mfano mdogo tu,japo muuzaji wa sokoni analipa ushuru lakini ushuru huo ni mdogo tu ambao hata mkulima anaweza kustahimili kuulipa.
Nilikuwa sijawahi kufanya kilimo chochote katika maisha yangu,ila nikadhamilia kuingia katika kilimo kwa lengo la kupata faida ya juu kabisa(maximum profit)ya kile ntakachozalisha.na wazo langu likanipeleka kufanya kilimo cha matikiti maji.na sababu ya kuchagua matikiti maji ni kama ifuatavyo: kwanza kabisa yanakomaa kwa muda mfupi,(miezi miwili hadi mitatu)hivyo sitasubili saana kupata faida yangu,pili ni matunda ambayo watu wengi wanayapenda,mimi nikiwa mmoja wao. Lakini pia nilitamani sana nisikosee,hivyo nilidhamilia kuhusisha wataaramu katika kila hatua ikiwa ni pamoja na kusoma kwenye mitandao habari mbalimbali zinazohusu kilimo cha matikiti maji. Nilifuata hatua zifuatazo:
HATUA YA KWANZA.
kutafuta shamba.
Hii ilikuwa ni hatua ya kutafuta shamba ,nilikwenda sehemu moja inaitwa usagala,nje kidogo ya jiji la mwanza na kukodi shamba la heka tatu kwa kiasi cha shilingi laki moja (kubargain muhimu) .kwa kuzingatia ukaribu na uwepo wa vyanzo vya maji.pia nilizingatia aina ya udongo kwa vile nilishajua matikiti maji yanastawi vizuri zaidi katika ardhi ya kichanga na sababu kubwa ikiwa ni kutotuamisha maji kwa ardhi ya kichanga.kwani maji yakiwa yanatuama husababisha matunda kuoza.

            Nikiwa shambani kuhakikisha kama linafaa kwa kilimo cha matikiti

Nikiwa tayari kwa ajiri ya maandalizi ya kilimo

HATUA YA PILI
Hii ilikuwa ni hatua ya kuandaa shamba,niliajiri wanakijiji wakalima eneo lote la heka tatu kwa kutumia maksai,pamoja na majembe ya mkono kwa ajili ya kupanga matuta.hatua hii ilinighalimu kiasi cha shilingi laki moja na nusu.hapa maksai wanatifua aldhi harafu majembe ya mkono yanatengeneza matuta(kama kawa nililia shida nikapunguziwa).

Ili  kazi iende vizuri nilifanya mpango tukawa tunapika chakula na kila mtu alikuwa anafurahi.hii inasaidia kupunguza movements wakati wa kazi,na pia inawatia moyo wafanyakazi na zaidi ikanijengea uhusiano mzuri na wao.wakati mwingine tatizo linaweza kutokea,wanakuwa upande wako.

HATUA YA TATU
upandaji
Katika ununuzi wa mbegu kwa mara ya kwanza ndo nilikutana na neno highbreed(mbegu chotara,zilizo tengenezwa kitaaram kutoa mazao mengi na bora)sikuweza kununua mbegu hizo kwa vile zilikuwa na gharama kubwa na mimi kwa vile ndo kilimo cha kwanza sikutaka kuingia gharama kubwa kwa kitu ambacho sijui matokeo yake(japo sikushauri ufanye kama mimi).niliamua kununua mbegu ya kawaida aina ya sugar baby,inayokomaa kwa siku sabini hadi themanini.pia matunda yake yanaukubwa wa wastani,hapa niligharamika kiasi cha shilingi elfu hamsini kwa ajiri ya manunuzi ya mbegu.katika upandaji tulikuwa tunaweka mbolea ya samadi iliyooza vizuri kwenye kila shimo na kuichanganya vizuri na udongo,tulihakikisha tuna panda mbegu mbili mbili kila shimo umbali wa sentimita mbili chini ya udongo kwa umbali wa sentimita 30 toka shina hadi shina na mita 1.5-2 kutoka mstari hadi mstari, kwavile wanakijiji washakuwa rafiki zangu walinipandia mbegu bila gharama yeyote,kuwaonesha ninajari nikaungurumisha ugali wa maana na dagaa za kutosha tukala tukashiba,na burudani za hapa na pale hazikukosa.




INAENDELEA....

16 comments:

  1. aisee nimeipenda sana naninandoto za kulima hiko kitu na dhani ndani ya mwaka huu huu naanza mchakato wa kulima hicho kitu ila nataka kujua mimi nipo pwani kunasehem moja inaitwa vikindu kusini mwa tanzania yatastawi na vipi kuhusu mbolea zinaulazima

    ReplyDelete
  2. Aisee kaka nimependa jinsji ulivyoielezea hiyo kazi ilivyofanyika ya kilimo cha matikiti maji hadi na mimi nimeshawishika kuanza hivi karibuni maana siku zote nilikuwa na ndoto na napenda itimie muda huu nilipoona wewe umeweza kufanya. Hivyo naona wewe ni kama "role model" wangu.

    ReplyDelete
  3. Kuna mchango wa kuifanya iendelee?

    ReplyDelete
    Replies
    1. poleni sana na samahanini sana hii blog ilisimama kwa muda lakini sasa iko hewani na tunaendelea na makala zetu ..kwa mara nyingine tena poleni kwa usumbufu

      Delete
  4. Tupe mwendelezo kaka, mafanikio na changamoto zake

    ReplyDelete
  5. vp mtokeo nini kilikushinda na nn ulifanikiwa?

    ReplyDelete
  6. Aisee nimeipenda hiyo kabla haijaisha...nami ngoja nijaribu

    ReplyDelete
  7. masoko yake yako wapi kaka? na vipi kuhusu east afria?

    ReplyDelete
  8. masoko yake yako wapi kaka? na vipi kuhusu east afria?

    ReplyDelete